Sawe atwaa ubingwa wa London,Jepkosgei amaliza wa pili

Ulikuwa ushindi wa pili kwa Sawe aliye na umri wa miaka 30, katika mbio za marathon baada ya kushinda mbio za Valencia marathon Disemba mwaka jana.

Dismas Otuke
1 Min Read

Sebastian Sawe alistahimili ukinzani mkali kabla ya kutwaa ushindi wa mbio za London Marathon leo kwa muda wa saa 2, dakika 2 na sekunde 27.

Ulikuwa ushindi wa pili kwa Sawe aliye na umri wa miaka 30, katika mbio za marathon baada ya kushinda mbio za Valencia marathon Disemba mwaka jana.

Jacob Kiplimo wa Uganda, aliyepigiwa upato kushinda, aliridhia nafasi ya pili kwa saa 2 dakika 3 na sekunde 57, huku Alexander Mitiso Munyao, akimaliza wa tatu kwa muda wa saa 2 dakika 4 na 20.

Bingwa mara nne wa London Marathon Eliud Kipchoge, aliambulia nafasi ya sita kwa saa 2, dakika 5 na sekunde 25 .

Joyciline Jepkosgei alishinda nishani ya fedha kwa muda wa saa 2, dakika 18 na sekunde 44 nyuma ya Tigst Assefa, wa Ethiopia, kwa saa 2, dakika 15 na sekunde 50, akivunja rekodi ya dunia kwa wanawake ya miaka 26 iliyopita ya Paula Radcliffe.

Sifan Hassan wa Uholanzi, alimaliza wa tatu kwa saa 2 dakika 19, huku Vivian Cheruiyot wa Kenya, akiridhia nafasi ya tano kwa saa 2 dakika 22 na sekunde 32.

Share This Article