Aliyekuwa Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, ameachiliwa huru wiki chache baada ya kuanza kuhutumikia kifungo cha miaka mitano gerezani.
Sarkozy alifungwa jela baada ya kupatikana na makosa ya uhalifu.
Sarkozy atakuwa chini ya uangalizi mkali wa mahakama na kuzuiwa kuondoka Ufaransa.
Tarehe 21 Oktoba rais huyo wa zamani wa mrengo wa kulia mwenye umri wa miaka 70, alihukumiwa kifungo cha miaka mitano kwa kula njama ya kufadhili kampeni yake ya uchaguzi wa 2007 kwa pesa kutoka kwa kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi.
Mawakili wake waliwasilisha ombi la kutaka aachiliwe, wakisubiri kesi ya rufaa itakayosikiliza mwezi Machi mwakani.
Akiongea na mahakama mjini Paris kwa njia ya video, Sarkozy alielezea muda wake katika kifungo cha upweke kama “uchungu” na “ndoto mbaya”.
Mwendesha mashtaka wa umma Damien Brunet alipendekeza kwamba ombi la Sarkozy la kuachiliwa likubaliwe, lakini rais huyo wa zamani apigwe marufuku kuwasiliana na mashahidi,
Sarkozy, ambaye amekuwa akikana kufanya kosa lolote, aliiambia mahakama kupitia njia ya video kwamba hajawahi kuwa na “wazo la kichaa” la kumuomba h marehemu Gaddafi pesa na kusema “sitakubali kitu ambacho sikufanya”.