Sanaa, muziki na michezo ni nguzo muhimu kuwaunganisha Wakenya licha ya migawanyiko mikubwa ya kisiasa na tofauti za kikabila.
Mashindano ya michezo ya kitaifa kwa shule na vyuo yaliyoandaliwa maajuzi katika kaunti ya Meru yaliashiria vipaji vya hali ya juu na kuunganisha matabaka mbalimbali.
Chuo kikuu cha Mount Kenya kilitawala tamasha hizo za kitaifa, kikishinda vitengo 17, na kumaliza katika nafasi ya pili katika vitengo 10 na pia kumaliza nafasi ya tatu katika vitengo vinane.
Chuo kikuu cha Kenyatta kilitawala tuzo hizo kikiibuka mabingwa wa jumla kwa mwaka wa tano mtawalia.
Washindi wa mashindano hayo wanawakilisha Kenya katika mashindano ya muziki ya Afrika Mashariki yanayoendelea mjini Kampala kuanzia Agosti 17 na yatakamilika tarehe 25 mwezi huu.