Sakaja: Uwanja wa Talanta upewe jina Raila Odinga

Tom Mathinji
1 Min Read
Uwanja wa Talanta.

Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja, amependekeza uwanja wa Talanta upewe jina la Raila Odinga, kwa heshima ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya hayati Raila Amollo Odinga.

Akizungumza wakati wa sherehe ya 62 ya Jamhuri katika uwanja wa Taifa wa Nyayo, Sakaja alitoa wito kwa Rais William Ruto kukubali uwanja huo upewe jina hilo.

Sakaja alimtaja Raila Odinga kuwa shujaa wa Nairobi aliyefanikisha Maendeleo mengi hasaa alipokuwa mbunge.

“Miongoni mwa mashujaa wa Nairobi alikuwa ni Raila Amollo Odinga. Baba, sisi kama watu wa Nairobi tunamuenzi. Alikuwa ni mbung aliyehudumu kwa muda mrefu. Kwetu sote, hii ndio Jamhuri ya kwanza bila Baba wetu. Tunaomba Mungu azidi kumlaza pema peponi na kile tunachoweza kufanya ni kuiga mfano aliyotuachia,” alisema Sakaja.

Uwanja wa michezo wa Talanta uko katika hatua za mwisho kabla ukamilike, huku ukitarajiwa kuandaa fainali za kombe la Mataifa bingwa Afrika, ambapo kenya itaanda kwa pamoja na Tanzania na Uganda.

Share This Article