Safari ya Kenya katika makala ya kwanza ya fainali za CHAN, ilifukia kikomo Ijumaa jioni baada ya kulemewa na Madagascar kwa penati 4-3, kufuatia sare ya bao moja katika muda wa kawaida katika robo fainali ya kwanza ugani Kasarani.
Harambee Stars waliotawala mechi hiyo walichukua uongozi mwanzoni mwa kipindi cha pili kupitia kwa
Alphonce Omija aliyeunganisha pasi ya Boniface Muchiri.
Hata hivyo wageni Barea kutoka Madagascar walirejea mchezoni kupitia penati ya Fenohasina Razafimaro kunako dakika ya 69.
Timu zote zilisalia na nguvu sawa baada ya dakika 120, na katika hatua ya matuta, Harambee Stars ikafunga tatu, nayo Madagascar ikafunga nne.