Serikali ya Rwanda imepiga marufuku mtaala wa elimu wa Ubelgiji uliokuwa unatumika katika shule ya Kigali, Ecole Belge.
Hatua hii inafuatia uamuzi wa mwezi jana wa serikali ya Rwanda kukatiza ushirikiano wa kidiplomasia na Ubelgiji ambao walitawala enzi za ukoloni.
Rwanda ilichukua hatua za kufunga ubalozi wake mjini Brussels baada ya kuishutumu Ubelgiji kwa kuingilia maswala yake ya ndani.