Rwanda: Mwanamitindo Moses Turahirwa akamatwa kwa matumizi ya dawa za Kulevya

Jared Ombui
1 Min Read
Moses Turahirwa.

Ofisi ya Upelelezi wa Jinai nchini Rwanda (RIB) imethibitisha kukamatwa kwa Moses Turahirwa, Mwanamitindo na mwanzilishi wa kampuni ya mavazi ya ‘Moshions’, kwa tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya.

Msemaji wa RIB, Thierry Murangira, alisema Turahirwa alikamatwa kwa tuhuma hizo, ambazo zilithibitishwa kupitia vipimo vilivyofanywa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kisayansi ya Rwanda (Rwanda Forensic Institute – RFI).

Murangira aliongeza kuwa uchunguzi bado unaendelea.

Hii sio mara ya kwanza kwa Turahirwa kukabiliwa na mashtaka ya aina hiyo. Mnamo Aprili 27, 2023, alikamatwa kwa tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya na kughushi nyaraka.

Julai mwaka wa 2023, Turahirwa aliachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Nyarugenge.

Share This Article