Ruto na Mudavadi wammiminia sifa tele marehemu askofu Sulumeti

Dismas Otuke
2 Min Read

Rais William Ruto na waziri mwenye mamlaka makuu serikalini Musalia Mudavadi wamemsifu aliyekuwa askofu mstaafu wa Jimbo katoliki la Kakamega Philip Sulumeti kwa mchango wake katika kukuza taifa.

Akihutubia waombolezaji katika misa ya wafu ya askofu huyo, kwenye Uga wa shule ya Approved mjini kakamega , Mudavadi ambaye alimwakilisha rais alisema kuwa rais anatambua mchango wa askofu huyo katika kukuza ukristo, ujio wa katiba mpya na ujenzi wa miundo msingi kama vile shule na hospitalii.

Kwa upande wake, Mudavadi alitambua kuwa askofu huyo alikuwa rafiki wake wa karibu ambaye walishauriana na kushirikiana katika maswala muhimu ya maendeleo ya jamii ya magharibi na hata taifa nzima.

Pia alifichua kuwa serikali itafungua ubalozi jijini Vatican kwa lengo la ushirikiano mwema baina ya Kenya na uongozi wa Vatican.

Misa hiyo pia ilihudhuriwa na gavana wa kaunti ya Kakamega ambaye alimsifu askofu huyo kwa ujenzi wa hospitali ya St.Mary’s Mumias na Mukumu na ushindi wa katiba mpya hivyo akawata wabunge kutimiza utekelezwaji wake.

Wengine waliohudhuria ni waziri wa biashara ndogo ndogo na vyama vya ushirika Wyclife Oparanya, mbunge wa Shinyalu Fred Ikana, Emmanuel Wangwe (Navakholo), seneta wa Busia Okiya Omtatah, askofu wa majimbo mbali mbali, mapadri na wengine wengi.

Baadaye, askofu huyo alizikwa katika kanisa kuu la Jimbo la Kakamega (St.Joseph Cathedral).

Share This Article