Rais William Ruto, anatarajiwa kufanya ziara nyingine eneo la Nyanza katika ngome ya kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga, katika juhudi za kutafuta uungwaji mkono katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Ruto atazuru kaunti ya Migori siku ya Jumapili na Jumatatu ijayo, Mei 4 na 5, kukagua miradi ya maendeleo iliyo chini ya usimamizi wa serikali ya kitaifa .
Katika ziara hiyo Rais, anatarajiwa kufanya mikutano ya hadhara na kujinadi katika maeneo bunge ya kaunti ya Migori ya; Suna East, Suna West, Uriri, Kuria West na Awendo.
Ruto amezuru eneo la Nyanza mara kadhaa tangu wafanye ukuruba na Raila mwaka jana.