Ruto awataka mashabiki wa Harambee Stars kudumisha nidhamu Jumapili

Pambano hilo litachezwa sambamba na lile kati ya DRC na Morocco, katika uwanja wa taifa wa Nyayo kuanzia saa tisa alasiri.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William  Ruto  amewasihi mashabiki wa timu ya taifa Harambee Stars, kudumisha nidhamu katika mechi ya mwisho ya kundi A kuwania kombe la CHAN dhidi ya Zambia, Jumapili hii katika uwanja wa Kasarani.

Ruto amekiri mchango mkubwa wa Harambee Stars kuliunganisha taifa kupitia kwa fainali za CHAN, lakini akawaomba mashabiki kuhakikisha taifa haliadhibiwi na shirikisho la kandanda Afrika CAF kwa ukiukaji wa sheria.

Aidha Rais amewataka mashabiki wasio na tiketi kutazama mechi hiyo kupitia runinga kwenye maeneo yaliyotengwa katika kaunti ya Nairobi.

Kenya inahitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kwanza kundini A, na kucheza robo fainali katika uwanja wa Kasarani.

Pambano hilo litachezwa sambamba na lile kati ya DRC na Morocco, katika uwanja wa taifa wa Nyayo kuanzia saa tisa alasiri.

Share This Article