Rais William Ruto amewasili jijini Yokohama nchini Japani ili kuhudhuria Kongamano la 9 la Kimataifa kuhusu Maendeleo ya Afrika – TICAD.
Ruto atahudhuria kongamano hilo linaloanza kesho Jumatano akilenga kutangaza Kenya kama kitovu muhimu cha biashara na uwekezaji barani Afrika.
Baadhi ya fursa ambazo Rais atanadi ni pamoja na miundombinu, maeneo maalum ya biashara, kilimo, rasilimali za nishati, na teknolojia ya habari na mawasiliano miongoni mwa zingine.
Rais ameandamana na Waziri wa Mambo ya Nje na pia Kiranja wa Mawaziri Musalia Mudavadio miongoni mwa maafisa wengine wakuu serikalini.