Rais William Ruto amewasili kaunti ya Mombasa Jumamosi jioni tayari kuongoza sherehe za mwaka huu za Mashujaa zitakazoandaliwa kesho Jumapili katika kaunti ya Kwale.
Punde baada ya kuwasili, Ruto akiandamana na mkewe Rachael, walilakiwa na Waziri wa Biashara Salim Mvurya.
Rais anatarajiwa kuongoza taifa kwa sherehe zitakazoandaliwa katika kaunti ya Kwale kwa mara ya kwanza.
Matayisho tayari yamekamilika huku zaidi ya mashujaa 140, wengi wao kutoka Pwani, wakitarajiwa kutambuliwa.