Rais William Ruto amewasili katika kaunti ya Migori mapema Jumapili,kwa ziara ya siku tatu; anakotarajiwa kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzindua miradi mipya.
Ruto amelakiwa na viongozi wakuu serikalini kutoka eneo hilo punde alipowasili katika shule ya msingi ya Kadika eneo bunge la Suna East, wakiwemo Mawaziri kutoka eneo la Nyanza, Cabinet Opiyo Wandayi wa kawi, John Mbadi wa Hazina kuu na Katibu wa usalama wa ndani Raymond Omollo.
Viongozi wengine waliomlaki Ruto ni Gavana wa Migori Ochillo Ayacko, Seneta wa Kisumu Tom Ojienda, na kiongozi wa wachache bungeni Junet Mohamed.
Ruto anatarajiwa kuzindua ujenzi wa taasi ya kiufundi na kufungua afisi ya Naibu Kaunti Kamishna eneo la Piny Oyie katika eneo bunge la Suna West.
Kesho Rais atakagua soko la Kosir ESP na kuzomdua jengo katika shule ya Rongo Comprehensive School na baadaye kuhudhuria mikutano ya hadhara mjini Rongo.
Jumanne Rais atakagua soko la Ntimaru ESP na ujenzi wa nyumba za gharama nafuu mjini Ntimaru .