Rais William Ruto Ijumaa Adhuhuri amelipokea rasmi Kombe la kifahari la Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya (UEFA), katika Ikulu ya Nairobi.
Akizungumza punde katika hafla hiyo Ruto alisema kuwa Kenya ina talanta nyingi zinazopaswa kukuzwa kupitia kueka miundo mbinu bora.
Rais alisisitiza kuwa serikali yake itaendelea kuwekeza katika sekta ya michezo wakiiga mifano kutoka kwa mataifa yanayofanya vyema katika ngazi ya kimataifa katika soka.
Kiungo wa zamani wa Manchester United na Bayern Munch Bastian Schweinsteiger anaongoza ziara ya Kombe hilo litakalozungushwa katika mataifa matano ya Kenya,Vietnam,Afrika Kusini,Indonesia na Zambia.