Ruto akutana na Waziri Mkuu wa Japani Shigeru Ishiba, wajadili ushirikiano

Viongozi hao wawili walikutana kwenye kikao cha faragha mjini Yokohama, pembezoni mwa Kongamano la Tisa la Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika – TICAD 9.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto mapema leo Jumatano amekutana na Waziri Mkuu wa Japani Shigeru Ishiba na kujadiliana kuhusu ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali.

Ruto alielezea haja ya Japani kuondoa vizuizi vya ushuru wa forodha na vile visivyokuwa vya ushuru wa forodha ili kuongeza bidhaa za Kenya zinazouzwa nchini Japani kama vile maparachichi, chai na mazao mengine.

“Kenya na Japani zina ushirikiano mzuri na thabiti ambao umedumu kwa kipindi cha miaka 60 iliyopita. Biashara yetu imekua kwa kiwango kikubwa kwa kipindi hicho, huku biashara ikikua kwa asilimia 33 mnamo mwaka 2024. Hata hivyo, ushirikiano wa biashara kwa kiwango kikubwa unaipendelea Japani,” alisema Ruto wakati wa mkutano huo.

Viongozi hao wawili walikutana kwenye kikao cha faragha mjini Yokohama, pembezoni mwa Kongamano la Tisa la Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika – TICAD 9.

 

Share This Article