Ruto akutana na viongozi wa Afrika Ikulu kujadili mageuzi ya Umoja wa Afrika, AU

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amekutana na viongozi kadhaa kutoka barani Afrika kujadili mageuzi ya Umoja wa Afrika, AU.

Kwenye hotuba yake, Ruto alisema kuwa kikao hicho kiliafikiana kuimarisha utendakazi wa mahakama ya kisheria  ya AU.

Aidha, viongozi hao walisema ipo haja ya umoja huo kuratibu upya mfumo wa kudumisha amani na kusuluhisha mizozo.

Ruto alielezea kutamaushwa kwake na hali ilivyo mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, na kusema  wamepanga  kikao  na  viongozi  wengine  kutoka  Jumuiya  ya Afrika  Mashariki  kesho  kutwa, ili  kujadiliana na Rais Paul Kagame wa Rwanda na pia  Rais Felis Tshisekedi wa DRC jinsi ya kutafuta suluhu.

Viongozi waliohudhuria kongamano hilo ni pamoja na Marais Azali Assoumani wa Comoros, Général Umaro El Mokhtar Sissoco Embalo wa Guinea-Bissau, Taye Selassie kutoka Ethiopia, na John Dramani Mahama wa Ghana, pamoja na Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat.

Share This Article