Ruto ahudhuria ufunguzi wa bwawa la Grand Ethiopian Renaissance

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto siku ya Jumanne alikuwa miongoni mwa viongozi waliohudhuria ufunguzi wa bwawa la Grand Ethiopian Renaissance.

Ruto alijumuika na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.

Bwawa hilo lililojengwa na serikali ya Ethiopia litakuwa kubwa zaidi barani Afrika kuzalisha umeme unaokadiriwa kuwa megawati 6,450.

Ruto amesema Kenya iko tayari kusaini mwafaka wa makubaliano wa kununua umeme kutoka Ethiopia utakaotumika viwandani, vyuo vya teknolojia ya habari na mawasiliano na viwanda vya uchakataji mazao ya kilimo.

Share This Article