Ruto afanya uteuzi wa wenyekiti wa mashirika ya umma

Dismas Otuke
1 Min Read
Rais William Ruto.

Rais William Ruto amefanya uteuzi wa wenyekiti wa mashirika kadhaa ya humu nchini kwa kipindi cha miaka mitatu.

Uteuzi huo ni katika utumishi wa umma,mashirika ya serikali,mamlaka ya biashara ndogo na za kadri za kibiashara,mamlaka ya raslimali za maji,shirika  la madini nchini na shirika la kupambana na ulaji muku nchini ADAK.

Kupitia gazeti rasmi la serikali la Oktoba 4,Ruto amewateua wanachama wa tume ya utumishi wa umma wakiwa Arthur Osiya, Oscar Eredi, Nura Mohammed, Grace Kamau, Ruth Ruraa, Nancy Butama na Elizabeth Chesang .

Victor Munyaka ameteuliwa mwenyekiti wa kituo za uzalishaji mifugo nchini, Kenya Animal Genetic Resource kwa muda wa miaka mitatu.

James Mureu ameteuliwa mwenyekiti wa mamlaka ya biashara ndogo na za kadri kwa kipindi cha miaka mitatu, huku Donald Murgor akiteuliwa mwenyekiti wa mamlaka ya raslimali za maji pia kwa miaka mitatu.

Katika uteuzi mwingine Silas Jonyo ndiye mwenyekiti wa baraza la taasisi ya mawasiliano nchini, wakati Joseph Lagat akiteuliwa mwenyekiti wa Shirika la madini nchini .

Askofu Joseph Kagunda ameteuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa shirika la kupambana na ulaji muku nchini-ADAK.

Share This Article