Rais William Ruto amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kabla ya kuandaliwa kwa Mkutano wa Mifumo ya Chakula wa Umoja wa Mataifa, UN.
Mkutano kati yao ulifanyika katika Ikulu ya Taifa hilo.
Rais Ruto akitumia fursa hiyo kusifia uhusiano mzuri ambao umekuwepo kati ya nchi hizo mbili.
“Kenya na Ethiopia zinashirikishana uhusiano thabiti na wa kihistoria uliojikita katika ujirani mwema na uhusiano thabiti wa kidiplomasia. Uhusiano huu wa muda mrefu umetawaliwa na sifa ya heshima na ushirikiano wa pande mbili, kukuza uthabiti na ushirikiano katika Pembe ya Afrika,” alisema Rais Ruto baada ya mkutano wao.
“Uhusiano wetu umejikita kwenye Makubaliano ya Hadhi Maalum yaliyotiwa saini mnamo mwaka 2012, na ambayo yanahudumu kama mpangokazi wa ushirikiano ulioboreshwa katika uendelezaji wa miundombinu, nishati, biashara na uwekezaji, na utangamano wa kikanda.”