Rais William Ruto ameondoka mapema leo Jumapili kuelekea mjini Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria kongamano la pili la Afrika kuhusu mazingira.
Kongamano hilo la Marais linalenga kutoa mwelekeo kuhusu mabadiliko ya tabianchi kufuatilia kwa maazimio ya Nairobi mwaka 2023.
Ruto pia atashuhudia kusainiwa kwa mwafaka wa ushirikiano wa matumizi ya akwi safi viwandani barani Afrika AGII, ukishirikisha serikali za Afrika, wafadhili na shirika la biashara huru Afrika AfCFTA na waekezaji wa kibinafsi.
Aidha Rais atakuwa mgeni wa heshima katika hafla ya kufungua bwawa la Grand Ethiopian Renaissance litakalotumiwa kuzalisha umeme.