Ruto aagiza kuachiliwa kwa pikipiki zinazozuiliwa katika vituo vya polisi

Pikipiki zitakazoachiliwa huru ni zile ambazo hazikuhusika katika visa vya uhalifu. Wizara ya Usalama wa Taifa na Inspekta Mkuu wa Polisi wametakiwa kuhakikisha hilo linafanyika.

Martin Mwanje
1 Min Read

Wahudumu ambao pikipiki zao zinazuiliwa katika vituo mbalimbali vya polisi kote nchini, na pikipiki hizo hazikuhusika katika visa vya uhalifu wana kila sababu ya kutabasamu. 

Hii ni baada ya Rais William Ruto kuagiza kuachiliwa kwa pikipiki hizo katika kipindi cha siku saba zijazo.

“Nimetoa msamaha kwa wamiliki wa pikipiki zinazozuiliwa katika vituo vya polisi na hazikuhusika katika visa vya uhalifu,” alisema Rais Ruto alipokutana na maafisa wa bodaboda katika Ikulu ya Nairobi leo Alhamisi.

“Nimeitaka Wizara ya Usalama wa Ndani kufanya kazi na Inspemkta Mkuu wa Polisi kuachilia pikipiki hizo katika kipindi cha wiki moja ijayo.”

Ruto akitumia fursa hiyo kusisitiza kuwa wahudumu wa bodaboda ni wawekezaji halali ambao biashara zao zinapaswa kuungwa mkono.

Ameahidi kufanya kazi na wadau wote kutekeleza sheria itakayowawezesha wahudumu hao kujidhibiti ili kuchochea ukuaji wa sekta hiyo.

 

 

 

 

Share This Article