Ruth Matete alalamikia wanaomkosoa kuhusu marehemu mume wake

Alichapisha ujumbe aliopokea kutoka kwa mtu ambaye hakumtaja anayemlaumu kwa kutochapisha hata jumbe za kukumbuka mume wake.

Marion Bosire
2 Min Read
Ruth Matete

Mwimbaji wa nyimbo za injili ambaye pia ni mhubiri Ruth Matete amelalamika kuhusu watu ambao wanamkoosoa kuhusu kifo cha mume wake Beloved John Apewajoye.

Kwenye Insta Stories, msanii huyo alichapisha jumbe za mkosoaji mmoja na kuandika, “Miaka mitano baadaye na bado hawajanisamehe kwa kitu ambacho sikukifanya. Nimechoka kuwa mwenye nguvu.”

“Ninafaa kufanya nini? Niandae sherehe kila mwaka ya kukumbuka kifo cha mume wangu? aliendelea kusema mama huyo wa mtoto mmoja binti kwa jina Toluwa.

Katika ujumbe huo aliotumiwa, hakuonyesha aliyemtumia lakini mtu huyo anashangaa jinsi Ruth anishi maisha yake na binti yake bila kumkumbuka mume wake kana kwamba alikuwa kosa kwenye maisha yake.

“Ruth! Ona jinsi unaishi maisha yako na binti yako bila kumbukumbu ya ina yoyote ya Beloved John Apewajoye.” aliandika mtu huyo akishangaa ni kwa nini Ruth huwa hachapishi hata jumbe za kukumbuka mume wake kwenye mitandao ya kijamii.

Aliendelea kumshauri awe na utu hata ingawa wanajua hakumpenda mwendazake huku akimlaumu kwa kumtoa kwa watu ambao walimpenda na kumuenzi.

“Una damu yake maishani mwako na huwa unaionyesha hadharani (Toluwa) utadhani ni wako peke yako. Pastor Ruth Matete Apewajoye.” aliendelea kusema mkosoaji huyo.

Mume wa Ruth Matete ambaye alikuwa mhubiri kwa jina Beloved John Apewajoye alifariki Aprili 11, 2020, baada ya kulazwa katika hospitali kuu ya Kenyatta.

Alikuwa na majeraha mabaya ya moto uliotokana na kile kilichotajwa kuwa mlipuko wa mtungi wa gesi ya kupikia katika nyumba yao huko Athi River.

Watu wa familia yake hawakuweza kuhudhuria mazishi yake katika makaburi ya Lang’ata jijini Nairobi kwani wakati huo janga la Corona lilikuwa limesababisha kuwekwa kwa vikwazo vya usafiri kote ulimwenguni.

Share This Article