Ruth Chepng’etich na Peres Jepchirchir wajiondoa London Marathon

Tom Mathinji
1 Min Read
Ruth Chepng'etich.

Mshikilizi wa rekodi ya dunia Ruth Chepngetich pamoja na bingwa mtetezi Peres Jepchirchir, wamejiondoa katika mbio za Marathoni za London, zitakazoandaliwa wikendi ijayo.

Chepngetich, mwenye umri wa miaka 30, alikuwa mwanariadha wa kwanza wa kike kumaliza mbio za marathoni chini ya muda wa saa mbili, dakika kumi aliposhinda mbio za marathoni za Chicago mwaka 2024, lakini akadokeza kuwa hayuko tayari kwa mbio za London mwishoni mwa juma lijalo.

“Nina huzuni sana kukosa mbio hizo, lakini nitarejea kwenye mbio za London Marathon mwaka 2026,” alisema Chepng’etich.

Siko tayari kimwili na pia kiakili kushiriki mbio hizo, kwa hivyo najiondoa,’ aliongeza mwanariadha huyo.

Kwa upande mwingine, Jepchirchir, aliyeshinda mbio za London Marathon mwaka jana kwa muda wa saa mbili, dakika 16 na sekunde 16, hatashiriki mbio za mwaka huu kutokana na  jeraha la mguu.

“Kwa bahati mbaya, jeraha nililo nalo limesababisha nisishiriki , lakini natamia nitakuwa buheri wa afya hivi karibuni na kurejea kwa London Marathon nikiwa tayari,’ alisema mwanariadha huyo.

Kutokuwepo kwa Chepngetich na Jepchirchir katika mbio hizo, waandalizi wametangaza kuwa mwenzao Vivian Cheruiyot atakuwa na fursa nzuri katika mashindano hayo.

Cheruiyot, mwenye umri wa miaka 41, ameshiriki mbio za London mara tatu huku akishinda mwaka 2018.

Share This Article