Rekodi ya Dunia ya mita 5,000 ya muda wa dakika 13 sekunde 58.06, iliyoandikishwa na bingwa wa Olimpiki Beatrice Chebet wa Kenya imerasimishwa.
Chebet aliweka rekodi hiyo Julai 5 mwaka huu kwenye mashindano ya Prefontaine Classic mjini Eugene, Oregon nchini Marekani akiwa mwanamke wa kwanza kutimka mbio hizo chini ya muda wa dakika 14.
Chebet pia anashikilia rekodi ya Dunia ya mita 10,000 ya muda wa dakika 28 sekunde 54.14 na ile ya kilomita 5 ya dakika 13 na sekunde 54.