Rayvanny asema anaoa mwaka huu

Anapanga kumwoa mpenzi wake na mama ya mtoto wake Fahyma.

Marion Bosire
1 Min Read
Rayvanny

Raymond Shaban, mwanamuziki wa Tanzania ambaye wengi wanamfahamu kama Rayvanny ama Vanny Boy, ametangaza kwamba anaingia kwenye ndoa mwaka huu.

Vanny alitangaza hilo kupitia akaunti yake ya Instagram ambapo alichapisha picha ya mpenzi wake ambaye pia ni mke wake mtarajiwa Fahyma na kuandika, “Tamko rasmi naoa mwezi wa 5.”

Awali, chapisho hilo lilikuwa limeandikwa, “Kama nilikuchezea samahani, huyu ndiye mke wangu nampenda kuliko chochote kile, yeye ni kila kitu kwangu nampenda sana Fahyma maisha yangu. TAMKO RASMI NAOA MWEZI WA 5”.

Msanii huyo ambaye pia anamiliki kampuni ya muziki ya Next Level, baadaye alifuta maneno hayo ya kwanza na kubakisha tamko hilo linalosema anaoa mwezi wa 5.

Rayvanny na Fahyma wamekuwa wapenzi kwa muda mrefu lakini walitengana kwa muda wa miaka mitatu kabla ya kurudiana tena mwaka 2023.

Kipindi ambacho alikuwa ameachana na Fahyma, Rayvanny alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Paula Kajala, uhusiano uliofikia mwisho Septemba 2022.

Rayvanny na Fahyma wana mtoto mmoja wa kiume.

Share This Article