Ratiba ya kwota fainali kuwania kombe la Afrika kwa wanawake imekamilika kufuatia kumalizika kwa mechi za makundi zilizochezwa jana usiku nchini Morocco.
Mabingwa mara tisa Nigeria walioongoza kundi B watachuana na Zambia, waliomaliza wa pili kundini A, Julai 18, kuanzia saa moja usiku, kabla ya kuwapisha viongozi wa kundi A, Morocco, watakaochuana na Mali iliyomaliza ya tatu kutoka kundi C.
Jumamosi Julai 19, Algeria iliyomaliza ya pili kundini B, itacheza dhidi ya Mali, iliyomaliza ya tatu katika kundi C kuanzia saa moja usiku, kisha mabingwa watetezi Afrika Kusini wamalize udhia na Senegal.