Ratiba ya mechi za robo fainali kuwania kombe la mataifa ya Afrika (AFCON), kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20 itabainika leo baada ya mechi za mwisho za makundi.
Mechi za mwisho mbili za kundi A zitasakatwa leo, Afrika Kusini ikipambana na Zambia wakati wenyeji Misri wakichuana na Tanzania.
Sierra Leone inayoongoza kundi hilo tayari imefuzu kwa kwota fainali ikiwa na alama saba, moja zaidi ya Afrika Kusini huku Zambia na Misri zikiwa na alama 5 na 4 mtawalia.
Wenyeji ni sharti waishinde Tanzania ili kufuzu kwa robo fainali.
Tim timu zilizofuzu kwa hatua ya nane bora ni Sierra Leone, Morocco, Nigeria, Ghana na mabingwa watetezi Senegal.
Tim nne bora katika kipute hicho zitafuzu kushiriki Kombe la dunia kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20 kati ya Septemba na Oktoba mwaka huu nchini Chile.