Rais Yoweri Museveni kufanya ziara rasmi nchini Kenya

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais wa Uganda Yoweri Museveni kufanya ziara rasmi nchini Kenya.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, anatarajiwa kuwasili hapa nchini leo Jumatano, kwa ziara rasmi ya kiserikali.

Atakapowasili, Museveni atalakiwa na mwenyeji wake Rais  William Ruto katika Ikulu ya Nairobi, ambapo viongozi hao wawili watajadili maswala muhimu kuhusu uhusiano kati ya Kenya na Uganda.

Aidha mazungumzo kati ya viongozi hao wawili, yatalenga kuimarisha utangamano wa kanda hii, amani katika kanda ya Afrika Mashariki pamoja na kutafuta fursa mpya za ushirikiano.

Baadaye viongozi hao wawili wataandaa mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari, katika Ikulu ya Nairobi.

Share This Article