Rais William Ruto kuongoza sherehe za 62 za Madaraka huko Homa Bay Leo

Kauli Mbiu ya mwaka huu ya sherehe za Madaraka inahusu Uchumi wa Samawati na shughuli za baharini.

Marion Bosire
1 Min Read
Rais William Ruto.

Rais wa Jamhuri ya Kenya William Ruto leo anatarajiwa kuongoza sherehe za 62 za Madaraka Day leo katika uwanja wa michezo wa Raila Odinga katika kaunti ya Homa Bay.

Kiongozi wa nchi amekuwa katika eneo hilo kwa muda wa siku kadhaa kuanzia Alhamisi huku sherehe hizo ambazo kauli mbiu yake inaangazia uchumi samawati zikiandaliwa.

Alikagua miradi mbali mbali katika eneo hilo pamoja na kufunga kongamano lililokuwa likiendelea kuhusu Uchumi Samawati katika chuo kikuu cha Tom Mboya.

Wakenya wa matabaka mbali mbali tayari wamefurika katika uwanja huo wa Raila Odinga kushuhudia sherehe za mwaka huu ambazo zinaandaliwa humo kwa mara ya kwanza kabisa, wengine wakiripotiwa kukesha humo.

Uwanja huo unaweza tu kumudu watu elfu 12 na kutokana na hilo inaripotiwa kwamba kuna wakenya wengi ambao hawajapata fursa ya kuingia humo.

Msemaji wa serikali Isaac Mwaura alisema kwamba kaunti ya Homa Bay ilichaguliwa makusudi kuandaa sherehe za mwaka huu kama njia ya kuonyesha umuhimu wake katika uchumi samawati nchini kuambatana na kauli mbiu ya mwaka huu.

Akizungumza jana katika chuo kikuu cha Tom Mboya, Mwaura alisema kwamba kaunti ya Homa Bay iko katika eneo zuri, kwenye fuo za Ziwa Viktoria.

Share This Article