Rais wa Senegal, Waziri Mkuu wa Msumbiji wamwomboleza Raila

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais Ruto amkaribisha Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye.

Rais wa Senegal President Bassirou Diomaye Faye na Waziri Mkuu wa Msumbiji  wametuma rambirambi kwa wananchi wa Kenya kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga.

Akizungumza katika uwanja wa Ithookwe kaunti ya Kitui wakati wa maadhimisho ya Siku Kuu ya Mashujaa, Rais Faye alimtaja Raila kuwa kiongozi shupavu wa kisiasa.

Faye, ambaye ndiye mgeni wa heshima wa sherehe za Mashujaa mwaka huu, alituma rambirambi zake za kibinafsi kwa Rais William Ruto na kwa familia ya Odinga.

“Nachukua fursa hii kuleta rambirambi za watu wa Senegal kwa watu wa kenya kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga,” alisema Rais Faye.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Msumbiji, alimkumbuka Raila kuwa mzalendo wa kipekee, akidokeza kuwa atakoswa sio tu nchini Kenya lakini katika Bara nzima la Afrika.

“Bara la Afrika limempoteza mzalendo wa kipekee. Huu ni wakati wa kuheshimu matendo ya wale waliojitoa mhanga kuleta ukombozi na ujenzi wa taifa,” alisema Maria Benvinda Levy,

Share This Article