Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Diakhar Faye amewasili jijini Nairobi Jumapili jioni tayari kuhudhuria sherehe za siku kuu ya Mashujaa siku ya Jumatatu katika kaunti ya Kitui.
Rais Faye atakuwa mgeni wa heshima huku pia akitarajiwa kusaini mikataba kadhaa ya ushirikiano baina ya Kenya na Senegal.
Faye amelakiwa katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta na Waziri wa Michezo Salim Mvurya.
Rais William Ruto anatarajiwa kuongoza sherehe hizo zitakazoandaliwa katika uwanja Ithookwe kaunti ya Kitui.