Rais Samia wafanya mazungumzo na Rais Stubb wa Finland

Stubb alitokea Kenya alifanya mazungumzo na kusaini mikataba kadhaa ya ushirikiano na Rais William Ruto.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, jana Mei 14, alifanya kikao cha mazungumzo na Rais wa Finland, Alexander Stubb, katika Ikulu ya Dares Salaam, alipowasili kwa ziara rasmi ya kiserikali ya siku tatu.

Stubb alitokea Kenya alifanya mazungumzo na kusaini mikataba kadhaa ya ushirikiano na Rais William Ruto.

Tanzania na Finland zina ushirikiano wa karibu wa miaka 60, katika sekta za elimu, mabadiliko katika mifumo ya kodi, misitu, ulinzi, uchumi wa majini, akili mnemba, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na usawa wa kijinsia.

Share This Article