Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kujenga ukumbi wa kisasa wa tamasha za muziki kushindana na ule wa Kigali Arena nchini Rwanda.
Rais Samia anaonekana kuitikia ombi la wasanii kama vile Diamond Platinumz, ambao walimwomba kuwajengea ukumbi wa kisasa wa kupiga tamasha.
Samia ametenga bajeti ya shilingi bilioni 22.2 za Kenya, sawia na dola milioni 172 kwa ujenzi wa ukumbi huo.
Ukumbi wa Kigali Arena ulijengwa mwaka 2019 na serikali ya Rwanda, na hutumika kuandaa mashindano ya ukumbini pamoja na tamasha.