Rais Samia azindua ujenzi wa makao makuu ya CCM

Chama hicho cha CCM kinajiandaa pia kwa mkutano mkuu utakaofanyika kesho na Ijumaa jijini Dodoma.

Marion Bosire
2 Min Read

Rais wa Tanzania Samia Suluhu hassan ambaye pia ni mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha Mapinzuzi CCM hii leo ameweka jiwe la msingi wa ujenzi wa makao makuu ya chama hicho tawala.

Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika katika eneo la Tambuka reli, Jijini Dodoma, litakapojengwa jengo hilo. Rais huyo alitangaza pia wito kwa wanachama wa CCM kuchanga hela kwa hiari kusaidia ujenzi huo.

Wananchi wengi walihudhuria hafla hiyo ambapo katika hotuba yake Rais Samia alisema, “Kupita mradi huu Chama chetu kinaenda kufungua sura mpya ya makao makuu yake na sote tunaweza kuwa sehemu ya kuifungua sura hiyo mpya.”

Kiongozi huyo alifichua kwamba ujenzi huo utagharimu shilingi bilioni 34 pesa za Tanzania akielezea kwamba sehemu ya ufadhili wa mradi huo utatoka kwa miradi tofauti ya chama wakutumai kujaliza na michango ya hiari ya wanachama.

Chama hicho cha CCM kinaendelea pia kujenga afisi zake za kimaeneo katika maeneo mbali mbali nchini Tanzania Rais Suluhu akiomba Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM isimamie zoezi hilo kwa karibu ili likamilike kwa wakati na ubora uliokusudiwa.

Hatua hii ya leo inajiri saa chache kabla ya mkutano mkuu wa chama cha CCM unaopangiwa kuandaliwa Mei 29 na 30 huko Dodoma.

Kati ya masuala yanayotarajiwa katika kongamano hilo ni uzinduzi wa ilani ya kuongoza taifa la Tanzania kwa miaka mitano ijayo.

Tanzania inatarajiwa kuandaa uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huuna Rais Samia ndiye atakayepeperusha bendera ya chama cha CCM katika kinyang’anyiro hicho.

Share This Article