Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameunda tume huru ya kuchunguza matukio yaliyoshuhudia siku ya uchaguzi Oktoba 29, 2025 na siku kadhaa baadaye.
Katika taarifa rasmi kwa umma, Rais Samia alielezea kwamba alibuni tume hiyo kulingana na madaraka aliyokabidhiwa kisheria chini ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32.
Alimteua Mohamed Chande Othman ambaye ni Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo na wajumbe wakiwa Ombeni Yohana Sefue ambaye ni mwanadiplomasia na Balozi Radhia Msuya.
Wengine ni Paula Meela mwKatika taarifa rasmi kwa umma, Rais Samia alielezea kwamba alibuni tume hiyo kulingana na madaraka aliyokabidhiwa kisheria chini ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32.anadiplomasia na balozi mstaafu, Said Ali Mwema ambaye alikuwa mkuu wa jeshi awali, David Kapya mwanadiplomasia na Balozi mstaafu huku Stergomena Lawrence Tax akifunga orodha.
Haya yanajiri wakati ambapo miito imetolewa ya maridhiano katika taifa hilo la Afrika mashariki kufuatia uchaguzi ulioghubikwa na utata.
Wafuasi sugu wa upinzani hata hivyo wanakataa juhudi za maridhiano wakitaja serikali ya sasa ya chama cha CCM kuwa isiyo halali kwani uchaguzi haukufanyika.
Vijana wengi wanaripotiwa kuuawa kwenye makabiliano na maafisa wa usalama kwenye maandamano ya kulalamikia dosari za uchaguzi.