Rais Samia aongoza uapisho wa Jaji Mkuu George Masaju

Aliteuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na Rais Samia Suluhu Juni 13, kumrithi Professa Ibrahim Juma aliyestaafu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, siku ya Jumapili, ameongoza uapisho wa Jaji George Mcheche Masaju kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Awali Masaju alikuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Tanzania hadi Februari mosi mwaka 2018, baada ya kuhudumu kwa miaka mitatu chini ya setikali ya Rais Jakaya Kikwete.

Aliteuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na Rais Samia Suluhu Juni 13, kumrithi Professa Ibrahim Juma aliyestaafu.

Share This Article