Rais Ruto: Tunaondoa mitaa duni kupitia nyumba za bei nafuu

Tom Mathinji
1 Min Read
Nyumba za bei nafuu.

Rais William Ruto amesema kuwa serikali yake imejitolea kubadilisha mtaa wa Kibra kutoka mtaa duni hadi mtaa wa kisasa.

Akizungumza siku ya Ijumaa alipokagua ujenzi wa nyumba za gharama nafuu katika mtaa wa Kibra Jijini Nairobi, kiongozi wa taifa alisema sura mpya ya mtaa wa Kibra itabadilisha maisha ya maelfu ya wakazi wake.

“Mpango wa kuondoa mtaa duni wa Kibra ni mojawepo wa miradi 200 ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zitakazoleta mabadiliko yanayosubiriwa na Wakenya,” alisema Rais Ruto.

Rais Ruto alisema utawala wake unaazimia kutoa nyumba salama, zenye hadhi na za bei nafuu kwa wakenya wote.

Kulingana na kiongozi huyo wa taifa, mtaa wa Kibra utakuwa na nyumba 4,500 za gharama nafuu.

Share This Article