Rais William Ruto Leo Jumamosi, ameelezea kujitolea kwake kuboresha maisha ya wakenya, akisema ametilia maanani maswala yaliyoibuliwa na Baraza la Maaskofu wa kabisa Katoliki kuhusu hali ya taifa.
Akizungumza wakati wa hafla ya kutawazwa kwa Askofu mteule Peter Kimani Ndung’u kuwa Askofu wa kanisa katoliki dayosisi ya Embu, kiongozi wa taifa alisema Makasisi hao waliibua maswala muhimu ya bima ya afya jamii, akihakikisha atayashughulikia.
“Nilipokea salamu kutoka kwa Baraza la Maaskofu wa kabisa katoliki Kupitia barua, kesho nitatafuta kanisa Katoliki ili wiki yangu iwe shwari,” alisema Rais Ruto.
Rais pia aligusia juhudi zinazoendelea za serikali kufanikisha mpito wa Gredi ya tisa, akisema ujenzi wa madarasa elfu 11 ya shule za sekondari msingi unakaribia kukamilika, kwa matumizi ya mwezi Januari mwaka ujao.
Pia alibainisha kuwa serikali iko katika harakati za kuajiri walimu zaidi ya elfu 20 ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.