Rais William Ruto ameondoka nchini kuelekea jijini Luanda nchini Angola ambapo atahudhuria mikutano miwili muhimu, haya ni kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed.
Katika taarifa hiyo, Mohamed alielezea kwamba Rais atahudhuria awamu ya saba ya mkutano wa pamoja kati ya umoja wa Afrika – AU na Umoja wa Uingereza – EU na mkutano wa kamati ya muda ya uangalizi kuhusu mabadiliko ya kitaasisi katika AU.
Kiongozi wa nchi atakuwa mwenyekiti wa mkutano huo wa pili akiwa bingwa wa Umoja wa Afrika kuhusu mabadiliko ya kitaasisi.
Viongozi watakaohudhuria mkutano wa AU na EU wataangazia ushirikiano kati ya mashirika hayo mawili wa muda wa miongo miwili na kushughulikia changamoto ibuka kama vile mabadiliko katika vipaumbele vya siasa za kimaeneo, pengo la ufadhili na vitisho vinavyoongezeka vya kiusalama.
Kenya itapendekeza vipaumbele ya ufadhili unaoweza kubashirika kwa mipango inayoongozwa na Afrika, mipango iliyoimarishwa ya kupambana na ugaidi na ushirikiano katika kuhakikisha usalama mipakani pamoja na hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Rais Ruto amapangiwa pia kushauriana na viongozi wa Uingereza kutafuta kupanua ushirikiano wa kibiashara, uwekezaji na utekelezaji wa mapatano ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Kenya na Umoja wa Uingereza.