Rais William Ruto leo Jumatano atafungua rasmi Kongamano la Ugatuzi linaloandaliwa katika kaunti ya Homa Bay.
Hilo ni kongamano la tisa kuandaliwa tangu kuasisiwa kwa mfumo wa ugatuzi nchini.
Ruto aliwasili katika kaunti ya Homa Bay jana Jumanne baada ya kuongoza hafla ya kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani iliyoandaliwa mjini Kakamega.
Kaulimbiu ya kongamano la mwaka huu ni “Kwa ajili ya Watu, Kwa ajili ya Ustawi: Ugatuzi kama Kichocheo cha Usawa, Ujumuishaji, na Haki katika Jamii.
Konagamano hilo la siku nne litakamilika Ijumaa wiki hii.
Linahudhuriwa na Magavana, Wabunge, Maseneta na Mawaziri miongoni mwa viongozi wengine mbalimbali.