Kenya na Uhispania zinashirikiana katika upanuzi wa fursa za biashara, uwekezaji na ubunifu wa nafasi zaidi za kazi kwa raia wa nchi hizo mbili.
Akizungumza nchini Uhispania alipokutana na Mfalme Felipe wa VI wa Uhispania Jijini Seville, Rais William Ruto alisema ushirikiano huo pia utajumuisha ubadilishanaji wa teknolojia katika kilimo ili kuimarisha utoshelevu wa chakula.
“Ushirikiano wa nchi hizi mbili utahusisha ubadilishanaji wa teknolojia kwenye kilimo ili kuimarisha utoshelevu wa chakula,” alisema Rais Ruto.
Kwa upande wake, Mfalme Felipe wa VI alielezea kujitolea kwa nchi yake kuunga mkono juhudi za kikanda za kufanikisha mageuzi katika mfumi wa ufadhili wa kimataifa.
Wakati huo huo, Rais Ruto alipongeza mkataba wa kimataifa wa ufanisi,watu na mazingira almaarufu 4P,akisema umeleta marekebisho ambayo yanajumuisha maenedeleo na maswala ya hali ya anga kuwa ajenda moja.
Akiongea wakati wa mkutano wa nne wa kimataifa kuhusu ufadhili wa maendeleo huko Seville,nchini Uhispania,rais Ruto alisema mkataba huo unahakikisha kuwa jamii ya kimataifa inakabili umaskini sawia na kulinda mazingira.
Aliwahimiza viongozi wa mataifa kushinikiza marekebisho kwenye mfumo wa kifedha wa kimataifa.