Rais Ruto: Kenya na Senegal zimeimarisha uhusiano wa kidiplomasia

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais Ruto akutana na Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, katika Ikulu ya Nairobi.

Rais William Ruto amesema kuwa Kenya na Senegal zina uhusiano ulioimarika Barani Afrika na duniani kote kwa Jumla.

Kiongozi wa taifa ameyasema hayo leo Ijumaa alipopokea ujumbe maalum kutoka Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye katika Ikulu ya Nairobi.

“Tumejitolea kuimarisha ushirikiano wetu katika sekta muhimu kwa ustawi wa nchi hizi mbili na raia wake kwa jumla,” alisema kiongozi wa taifa.

Ujumbe huo uliwasilishwa kwa Rais Ruto na Waziri wa Utangamano wa Afrika na Mambo ya Nje Yassine Fall.

Rais Ruto alisema nchi hizo mbili zitaendelea kutekeleza uhusiano wa kidiplomasia ulioimarika pamoja na kuimarisha juhudi za kuafikia malengo ya pamoja.

Share This Article