Rais Ruto azindua miradi kadhaa ya maendeleo Ukambani

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amekariri kujitolea kwa serikali kuzindua miradi ya maendeleo itakayowanufaisha wakazi wa eneo la Ukambani.

Aidha, alisisitiza kuwa serikali yake haitaacha eneo lolote au jamii yoyote nyuma humu nchini Kenya kimaendeleo.

Ruto amesema haya Jumatano alipokagua na kuanzisha miradi kadhaa ya maendeleo.

Alifichua kuwa serikali imetenga shilingi bilioni 1.5 kukarabati barabara katika kaunti ya Makueni huku kiwango kingine cha shilingi bilioni 9.3 zikitengewa kwa ujenzi wa bwawa la Thwake na na kiwango kingine cha shilingi bilioni 2 kwa kuunganisha umeme kwa nyumba zipatazo 18,000.

Akiwa Makueni Rais pia ameweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa soko la kisaa la shilingi milioni 350 eneo la Wote.

Aidha, ameanzisha ujenzi wa barabara ya umbali wa kilomita 20 ya Emali-Matiliku ikiwa sehemu ya barabara ya kilomita 42 ya Emali-Ukia, Ndundune, kaunti ya Makueni.

Barabaraba hiyo ya kima cha shilingi bilioni 1.1 itarahisha uchukuzi kwa kuunganisha maeneo ya Kativani, Manywani, Matiliku, Kalamba, Nziu, na masoko ya Ukia na mji wa Wote hadi Kajiado, Nairobi, na Mombasa.

 

 

 

 

Share This Article