Rais Ruto awatuza wanariadha walioshiriki mashindano ya Dunia,Tokyo

Dismas Otuke
2 Min Read

Rais William Ruto mapema Alhamisi amewatuza wanariadha walioshinda nishani kwenye mashindano ya Riadha Duniani mjini Tokyo, Japan mwezi uliopita.

Ruto aliandaa sherehe ya staftahi kwa kikosi chote kilichoshiriki mashindano ya Tokyo kikiongozwa na Kapteni Julius Yego.

Beatrice Chebet ambaye hakuwepo wakati wa hafla hiyo alituzwa shilingi  milioni 6  kwa kushinda medali mbili za dhahabu katika mita 5,000 na 10,000, huku Faith Kipyegon akipokea shilingi milioni 5 kwa kushinda  dhahabu ya mita 1500 na fedha ya mita 5,000.

Washindi wengine waliotuzwa ni Lillian Odira aliyenyakua dhahabu ya mita 800, Faith Cherotich aliyeshinda dhahabu ya mita 3,000 kuruka viunzi na maji, Emmanuel Wanyonyi aliyenyakua dhahabu ya mita 800 na Peres Jepchirchir aliyetwaa dhahabu ya marathoni.

Wengine ni Doracs Ewoi aliyeshinda fedha ya mita 1,500 na Edmund Serem na Raynold Cheruiyot walioshinda medali za shaba katika mita 3,000 kuruka viunzi na maji na mita 1,500 mtawalia.

Kila mshindi wa dhahabu alituzwa shilingi milioni 3,washindi wa fedha 2 na milioni 1 kwa walionyakua medali za shaba.

Kenya ilimaliza ya pili Duniani kwa medali 11, dhahabu 7, fedha 2 na shaba 2.

Kila mshindi wa dhahabu alituzwa shilingi milioni 3,washindi wa fedha 2 na milioni 1 kwa walionyakua medali za shaba.

 

 

Share This Article