Rais Ruto awateua upya Mwenyekiti na Makamishna wa IEBC

Tom Mathinji
1 Min Read
Erastus Edung Ethekon.

Rais William Ruto amewateua upya Mwenyekiti na Makamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), saa chache baada ya Mahakama Kuu kuharamisha uteuzi wao wa awali uliochapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali mnamo Juni 10,2025.

Uteuzi huo mpya uliochapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali Julai 10,2025, unajiri baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali kesi iliyowasilishwa kupinga uteuzi wa makamishna hao.

Katika uamuzi huo, majaji walitoa agizo kwa kiongozi wa taifa kuhalalisha uteuzi wa makamishna hao kwa kuchapisha upya majina yao kwenye gazeti rasmi la serikali, kabla hawajaapishwa.

Rais Ruto awateua upya Mwenyekiti na Makamishna wa IEBC.

Rais Ruto kupitia gazeti rasmi la serikali chapisho la Julai 10,2025, amemteua Erastus Edung Ethekon kuwa mwenyekiti huku  Ann Njeri Nderitu, Moses Alutalala Mukhwana, Mary Karen Sorobit, Hassan Noor Hassan, Francis Odhiambo Aduol na Fahima Araphat Abdallah wakiteuliwa wa makamishna wa IEBC.

Kulingana na ilani hiyo, Mwenyekiti na Makamishna hao watahudumu kwa kipindi kimoja cha miaka sita.

Uteuzi huo sasa unatoa fursa kwa mwenyekiti na makamishna hao kuapishwa na kuanza kutekeleza majukumu yao.

Share This Article