Rais Ruto awatakia Waislamu heri njema wanapoanza Ramadhan

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto awatakia Waislamu heri njema wakati wa mfungo wa Ramadhan.

Rais William Ruto ametuma ujumbe wa kheri njema kwa Waislamu kote nchini,wanapojiandaa kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Kwenye ukurasa wa X, Rais alisema mfungo wa Ramadhan unawapa waumini Waislamu fursa ya kipekee ya kukuza imani yao na kujitolea upya katika kautekeleza haki.

Aidha kiongozi wa taifa alisema mwezi wa Ramadhan unawapa Waislamu fursa ya kutafakari kuhusu mambo ya kiroho,kujitia nidhamu na kujitolea kutenda mema, kwa  kuwasaidia wasiojimudu katika jamii.

Kiongozi huyo wa taifa, aliishukuru jamii ya Waislamu humu nchini kwa mchango wao mkubwa katika ujenzi wa taifa hili, akiwahimiza kuendelea kuwasaidia wale ambao hawajabahatika katika jamii.

Ramadhan ni mwezi wa tisa katika kalenda ya waumini Waislamu, na unaaminika kuwa mwezi mtukufu zaidi.Ramadhan huanza na kuisha kwa kuandama kwa mwezi mpevu.

Share This Article