Rais Ruto awaongoza Wakenya kumuomboleza Jirongo

Tom Mathinji
1 Min Read

Rais William Ruto amewaongoza wakenya kumuomboleza aliyekuwa mbunge wa Lugari Cyrus Jirongo aliyeaga dunia Jumamosi asubuhi kwenye ajali ya barabarani.

Rais Ruto alimtaja Jirongo kuwa kiongozi aliyejitolea ambaye alijizatiti kukabiliana na changamoto za maisha.

” Nimehuzunishwa na kifo cha mbunge wa zamani wa Lugari Cyrus Jirongo. Alikuwa mwenye bidii, mfanyabiashara shupavu na aliyekabiliana na changamoto za kisiasa hapa nchini,”alisema Rais Ruto.

“Mawazo na maombi yangu nayaelekeza Kwa familia wakati huu mgumu wa majonzi,” aliongeza Rais Ruto.

Naye Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen alimwomboleza Jirongo akimtaja kiongozi aliyeacha urithi wa kisiasa na kibiashara wa kupigiwa mfano.

Spika wa bunge la Taifa Moses Wetang’ula, alisema Jirongo alikuwa kiongozi shupavu wa vijana katika miaka ya 90, ambao utasalia kwenye kumbukumbu za kisiasa hapa nchini.

Jirongo alifariki kwenye ajali ya barabarani Jumamosi asubuhi, kwenye barabara kuu ya Nakuru – Nairobi.

Share This Article