Rais Ruto awaomboleza waliofariki kwenye ajali Kisumu

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais Ruto awaomboleza waliofariki kwenye ajali Kisumu.

Rais William Ruto ametoa wito wa kuimarishwa kwa utekelezwaji wa kanuni za trafaiki, kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyotokea katika barabara kuu ya Kisumu–Kakamega siku ya Ijumaa.

Ajali hiyo iliyohusisha basi la shule ya upili ya Naki na ilisababisha vifo vya watu zaidi ya 20.

Kwenye taarifa Ijumaa jioni, Rais Ruto alituma rambirambi kwa jamaaa na marafiki wa walioangamia pamoja na wale waliojeruhiwa.

“Tunawaombea waathiriwa wa ajali hiyo iliyotokea Ijumaa usiku kwenye barabara Kuu ya Kisumu-Kakamega,” alisema Rais Ruto.

Kiongozi huyo wa taifa aidha, aliwataka maafisa wa polisi kumchukulia hatua yeyote atakayepatikana akivunja sheria za barabarani.

“Tunawaagiza maafisa wa trafiki kuwachukulia hatua wale wote wanaokiuka sheria na kusababisha ajali,ili kuhakikisha usalama barabarani kote nchini,” aliongeza kiongozi wa taifa.

TAGGED:
Share This Article