Rais Ruto atua Lodwar kwa sherehe za kitamaduni za Kiturkana

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto leo Ijumaa amewasili mjini Lodwar, kuhudhuria makala ya nane ya sherehe za kila mwaka za kitamaduni kwa jamii ya Waturkana, maarufu kama Tobong’u Lore.

Ruto anatarajiwa kufungua rasmi sherehe hizo leo ambazo hudumu kwa takbriban wiki moja kwa lengo la kusherehekea utamaduni na utalii wa jamii hiyo na zilianza jana.

Rais ameandamana na Mawaziri Beatrice Askul wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na waziri wa utalii bi Rebecca Miano.

Akihutubia umati mjini Lodwar, kiongozi wa taifa alipigia debe hatua yake ya kubuni serikali jumuishi,  alisema hiyo ni njia ya kuwashirikisha Wakenya kutoka pembe zote huku akiwakashifu wanaopinga hatua hiyo .

Share This Article