Rais William Ruto ametoa msaada wa vyakula, magodoro na blanketi kwa waathiriwa wa mkasa wa moto mtaani Kibera.
Ruto alitoa msaada huo baada ya kuhudhuria ibada ya kanisa la AIC Kibra, huku akitoa hakikisho la serikali kusimama na wote walioathiriwa.
Aidha, Rais alisema kuwa serikali itawapa ridhaa wote walioathiriwa na mkasa huo wa moto.
Moto huo uliozuka Jumamosi eneo la Makina ulisababisha hasara kubwa huku watu wanane wakiripotiwa kufariki, na zaidi ya 20 wakijeruhiwa vibaya.